16/01/2024
TWENDENI TWENDENI TUONE...!
Simba SC katika dirisha dogo la usajili wamefanya walichoamua kukifanya. Ni kipindi ambacho tumeshuudia maamuzi magumu zaidi kuweza kutokea katika SOKA la bongo.
Ni nani utamuamisha leo hii ya kwamba mwamba Luis Miquissone bado yupoo Sana msimbazi Ila General MOSSES PHILI kwa kheri.,,.Ni ngumu kumuamisha mtu ya kwamba Simba ingeachana na JEAN BALEKE ikiwa bado wanae ESSOMBA ONANA.
Katikati ya msimu mabadiliko ya washambuliaji wawili kidogo inaleta shida. Na ukizingatia ndio walikua chaguo la kwanza na la pili. Ukweli usiofichika ni kwamba uwezo wa BALEKE & MOSSES katika kufumania nyavu ulipungua kwa kiasi kikubwa. Ushahidi katika hili wao wote wawili kwenye kombe la mapinduz hawajafikisha goli tatu na wamecheza. Huenda hii ndio sababu iliyofanya Simba SC ku move on kutafuta majibu sahihi zaidi katika suala la umaliziaji.
Tumeletewa washambuliaji wawili kwaajili ya kuvaa majukumu ya MOSSES & BALEKE, wakisaidiwa na mkongwe JOHN BOCCO. Kwa aina ya usajili waliofanya kwa ujumla wake unaongeza balance ya timu kwa maana kuna kiungo wa chini pia kaongezwa. Kwa jinsi Simba SC wanavyocheza ikitokea usaji wa Hawa washambuliaji wawili ukalipa japo kwa 50% hakika nayaona mafanikio makubwa kwa Simba SC hususani kimataifa.