15/04/2026
BRRH YAENDELEA KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI
Idara ya Uzazi na Kizazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba (BRRH) leo Aprili 14, 2026 imefanya kikao muhimu cha MPDSR (Maternal and Perinatal Death Surveillance and Response) chenye lengo la kujadili kwa kina vifo vitokanavyo na uzazi, kubadilishana uzoefu, kuelekezana kitaalamu na kuweka mikakati madhubuti ya kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Akiongoza kikao hicho, Mkuu wa Idara ya Uzazi na Kizazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba, Dkt. Timon Theophil, amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji, ufuataji wa miongozo ya afya pamoja na ushirikiano wa karibu miongoni mwa wataalamu wa afya katika utoaji wa huduma bora kwa mama na mtoto, ili kukomesha vifo vitokanavyo na uzazi vinavyoweza kuzuilika. Kikao hicho kimewakutanisha wataalamu kutoka Idara ya Uzazi na Kizazi, ICU, Idara ya Dawa za Usingizi, Magonjwa ya Ndani, Idara ya Upasuaji pamoja na wataalamu wengine kwa mujibu wa muongozo wa kitaifa, hatua inayolenga kuimarisha mshik**ano wa kitaalamu katika kushughulikia changamoto za uzazi kwa ufanisi zaidi.
Kupitia kikao hiki, BRRH inaendelea kuonesha dhamira yake ya kuchambua changamoto za kitabibu, kuimarisha ushirikiano wa kitaalamu, kuboresha ubora wa huduma za uzazi na kupunguza, hatimaye kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi ambavyo vinaweza kuzuilika, k**a sehemu ya juhudi za kuimarisha afya ya mama na mtoto katika Mkoa wa Kagera.
โ๏ธAfisa habari Brrh Kagera