Teacher Jacob makweta

Teacher Jacob makweta Teacher Jb

26/05/2026

1.Professor Jay alizaliwa mwaka 1975, kwasasa ana umri wa miaka 50

2.Alianza muziki mwanzoni mwa miaka ya 1990s. Mwaka 1994 alijiunga katika kundi la Hard Blasters Crew, waliachia kazi mbalimbali ukiwemo Chemsha Bongo uliofanya vizuri

3.Mwaka 2001 alianza kazi k**a msanii anayejitegemea(solo artist), aliachia albamu yake ya kwanza ambayo humo ndani kulikuwa na nyimbo maarufu zikiwemo Bongo Dar es salaam, Piga Makofi na Ndio Mzee ambao ulifanya ashinde tuzo

4.Producer Master J aliweka wazi kwamba moja ya nyimbo bora alizowahi kutengeneza ni wimbo wa Bongo Dar es salaam wa mwanamuziki huyo wa hip hop

5. Mapinduzi Halisi ilikuwa albamu yake ya pili ambayo ilitoka 2003, ilishinda Kili Music Awards k**a albamu bora ya hip hop. Miongoni mwa nyimbo zilizopendwa zaidi ni Promota Anabeep, Msinitenge na Zali La Mentali ambao alioshirikiana na Juma Nature, Nargis Mohamed alianza kufahamika kupitia wimbo huu akiwa video queen kabla ya kufanya vizuri Miss Tanzania

6. Albamu nyingine alizotoa ambazo zilifanya vizuri ni pamoja na J.O.S.E.P.H ambayo moja ya nyimbo maarufu humo ni ule wa Nikusaidieje ulioshinda tuzo kadhaa. Albamu zake nyinginezo ni Aluta Continua, Izack Mangesho na Kazi Kazi ambazo pia zilikuwa na nyimbo zilizopokelewa vizuri

7.Professor Jay upitia nyimbo zake anatajwa kuwa msanii wa hip hop Tanzania aliyeweza kushawishi hata watu wenye umri mkubwa kufuatilia muziki huo kwani alikuwa na uandishi wa kipekee na wenye kubeba ujumbe unaogusa nyanja mbalimbali katika jamii

8.Ni miongoni mwa wanamuziki wachache nchini ambao wameweza kukubalika katika generations tofauti tofauti kutokana na kipaji na uwezo wake kisanaa

9.Kwa uwezo wake kimuziki, huwa anapewa heshima kubwa na wasanii wenzake sio tu Tanzania, hata nchi nyingine za Afrika mashariki ambako kazi zake zilifanya vizuri, kutumbuiza na kushirikiana na wanamuziki wa huko akiwemo Jose Chameleon wa Uganda

10. Sugu Joseph Mbilinyi na Lady Jay Dee(Jidee) ni miongoni mwa marafiki zake wa karibu katika tasnia pia walishirikiana kikazi nyakati tofauti

11. Katika maisha binafsi, Profesa Jay alifunga ndoa na Grace Mgonjo ambaye ni mshereheshaji(MC) anayefahamika, wana mtoto wa k**e mkubwa anayeitwa Lisa ambaye amefika elimu ya chuo kikuu. Jay ni mtu ambaye amekuwa akionekana kuwa karibu na familia yake ikiwemo kumpongeza binti yao kufanya vizuri kitaaluma

12. Mwaka 2015 professor Jay alishinda ubunge wa Mikumi akawa mmoja wa wanamuziki wachache walioshinda nafasi hiyo kupitia majimboni

02/04/2026

“Miezi sita haijaisha, ulikuwa unawaambia Watanzania wote wafanye kazi na waache kulalamika. Sasa muda wako wa kufanya kazi umefika, wewe ndiye unalalamika.”

“Arena, Watanzania wanahitaji elimu, afya, barabara na miradi ya maendeleo. Tunahitaji pia ndege zaidi na hospitali kila sehemu.”

“Mbolea kwa wakulima ni muhimu ili kuboresha maisha kwa ujumla.”

“Usijifikirie wewe na kundi dogo la wasanii, manesi, walimu na wengineo. Fanya kazi, lipa kodi, jenga, na ulipe mishahara ya wafanyakazi wako. Wanaomba sana na mara nyingi wanatuambia ‘samahani’ kwa kila kitu.”

“Ndugu yangu, studio yako ni nzuri, lakini Arena inasemekana itaanza kujengwa mwezi wa saba kulingana na tetesi nilizonazo. Mimi na wewe tunajua kuwa hizi ni siasa tu anazofanya.”

“Kwetu sisi, anaonekana ameomba jambo la maana, lakini serikali haionekani kutaka kulikubali. Majibu aliyopewa na viongozi mbalimbali, mbona hayazungumziwi?”

“Sote tunapenda muziki, lakini Arena si jambo la msingi sana kiasi cha kuifanya serikali ionekane haisikii.”

“Haya ni mawazo ambayo nina uhakika Dalwesh Momo ameyapitisha pamoja na jengo zima la Wasafi.”

“Ni jambo jema kwa tasnia ya muziki, lakini hii ndiyo changamoto ya kuwa mfalme. Hata hivyo, maisha yanaendelea.” - ujumbe wa Harmonize kwenda kwa Diamond.

25/03/2026

TANZIA

30/10/2024
06/07/2024

Katika hali isiyo ya kawaida mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina Frola Samson (12), mkazi wa wilaya ya Ilemela amepatikana baada ya msako wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza akiwa eneo la Buhongwa ambako alijificha yeye na mdogo wake aitwaye France Samson (8) huku akidanganya kuwa wametekwa na kutaka wazazi watume fedha ili waachiwe.

Inadaiwa kuwa watoto hao walitoweka nyumbani mnamo tarehe 4.7.2024, ambapo Frola aliiba pesa za Mama yake kiasi cha shilingi 150,000/= na kisha kutoweka na mdogo wake wakielekea Buhongwa ambako alianza kupiga simu kwa Mama yake mzazi akidai atumiwe pesa kwa ajili ya waliowateka ili wawaachie huru.

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kupokea taarifa na kufanya ufuatiliaji, limefanikiwa kuwapata watoto hao wakiwa salama huku wakiwa na simu, godoro na vyombo vingine vya matumizi ya ndani walivyonunua kwa kutumia pesa aliyoiba mtoto huyo.

22/05/2024

Mchezaji wa soka wa Tanzania Mmbwana Ally Samatta ambae anakupiga kwenye klabu ya PAOK ya nchini Ugiriki, amefanikiwa kutwaa taji la ligi Kuu ya Ugiriki akiwa na klabu hiyo (PAOK).

PAOK wametwaa Ubingwa wa ligi ya Ugiriki wakiwa na alama 80 kwenye jumla ya michezo 36 waliyocheza kwenye ligi wakiwaqcha nyuma kwa alama mbili AEK Athens ambao wameshika nafasi ya pili wakiwa na alama 78.

17/05/2024

Taarifa ya hali ya dawa za kulevya Duniani ya mwaka 2023 imeonesha kuwa takribani Watu milioni 219 walitumia bangi mwaka 2021, sawa na 4% ya idadi ya Watu duniani ambapo idadi hiyo imeongezeka kwa 21% katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Taarifa hiyo ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Nchini (DCEA) na kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma leo May 16,2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista J. Mhagama inaonesha kuwa matumizi ya bangi yanaendelea kuongezeka kwa kasi duniani kote na kwamba matumizi ya bangi yameendelea kuwa ya juu zaidi Amerika Kaskazini ambapo 17.4% ya Watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 walitumia bangi mwaka 2021.

Barani Afrika taarifa imeonesha kuwa Afrika Kaskazini ni kitovu cha biashara haramu ya bangi iliyosindikwa (cannabis resin) kuelekea Ulaya Magharibi na matumizi ya bangi ni ya juu katika Afrika Magharibi na Kati na kufikia mwaka 2021, karibu 10% ya Watu (milioni 30) waliripotiwa kutumia bangi katika kipindi cha mwaka 2020, hususan katika Nchi ya Nigeria.

Nchi nyingi Afrika zina uzalishaji wa bangi na imeendelea kuwa moja ya dawa inayosababisha athari kubwa miongoni mwa Watu wanaopatiwa matibabu ya uraibu.

17/05/2024

ENGLAND: Klabu zinazoshiriki Premier League zimeombwa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na Klabu ya Wolverhampton Wanderers inayopendekeza azimio la kupiga Kura ya kufuta Matumizi ya 'VAR' kuanzia Msimu ujao

Pendekezo hilo ambalo linadaiwa kupingwa na Bodi ya Ligi Kuu linatarajiwa kusikilizwa Juni 6, 2024 ambapo imeelezwa Bodi inatambua haki ya Wolves kutoa pendekezo hilo, lakini inadhani kufutwa kwa kunaweza kusababisha maamuzi mengi yasiyo sahihi

Aidha, baadhi ya Maafisa wa EPL wanadai pendekezo hilo litaathiri Ubora wa Ligi, pia kwa mujibu wa takwimu za Msimu huu zinaonesha kiwango cha maamuzi sahihi ya Uwanjani kimeongezeka kutoka 82% hadi 96 kupitia VAR

Soma https://jamii.app/VARAbolition

17/05/2024

Kutoka Huko tumekuletea hii. Achana na "Burj khalifa" Ambalo ni jengo Refu zaidi Duniani Kwa sasa likiwa na Mita zaidi ya 800+ kutoka Chini ya Ardhi kwenda juu

"Jeddah tower" hili ni limjengo likubwa sana linajengwa huko Saudi Arabia likikamilika litakuwa na Urefu wa kilometer (1) kutoka Ardhini kwenda juu Angani , hii ni hatari sana Litakuwa ni jengo Refu zaidi kujengwa duniani

Hebu subiri kwanza - ujue kilometer Moja ni parefu sana ?🤔
hili dude litakuwaje unadhani ? Hebu toa maoni yako kwenye comment je unaweza Kuishi juu kwenye jengo hili ?

Imeandikwa na 🖋️ " Mnyilinga - Max "

Address

Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Teacher Jacob makweta posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Teacher Jacob makweta:

Share