Famara Media

Famara Media Famara Media - Inform, Entertain and Educate.

Huu moto Arteta anaotengeneza mnauona? pale katikati yupo Declaine Rice, Bruno Grumaeles na Martin Odergard.....Shauri y...
08/08/2026

Huu moto Arteta anaotengeneza mnauona? pale katikati yupo Declaine Rice, Bruno Grumaeles na Martin Odergard.....Shauri yenu.

 ....... | Kiungo mkata umeme ndani ya . Mchezaji promising and she gives everything akiwa uwanjani.We are proud of you!...
08/08/2026

....... | Kiungo mkata umeme ndani ya .

Mchezaji promising and she gives everything akiwa uwanjani.

We are proud of you!! Keep on shinning.

MOSES KURIA AMPA CHANGAMOTO RIGATHI GACHAGUA KUAPA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA RUTOAliyewahi kuwa Waziri wa Huduma za Umma n...
08/08/2026

MOSES KURIA AMPA CHANGAMOTO RIGATHI GACHAGUA KUAPA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA RUTO

Aliyewahi kuwa Waziri wa Huduma za Umma nchini Kenya, Moses Kuria, amempa changamoto aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, kuweka wazi iwapo amewahi kufanya makubaliano yoyote ya kisiasa na Rais William Ruto.

Kuria amemtaka Gachagua kuomba miadi na Moderator wa Kanisa la PCEA, akifuatana na mke wake, Mchungaji Dorcas Rigathi, kisha mbele ya kamera ashike Biblia na kuapa kwamba hajafanya makubaliano yoyote na Rais William Ruto.

Katika changamoto hiyo, Kuria anamtaka Gachagua pia kuapa kwamba hatofanya makubaliano yoyote na Rais Ruto kabla ya tarehe 10 Agosti 2027, ikiwa ni kipindi ambacho Kenya itakuwa imeelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kuria amependekeza Gachagua atamke mbele ya Biblia kwamba iwapo kauli hizo si za kweli, basi amuombe Mungu Mwenyezi amwadhibu kwa radi na umeme.

Akihitimisha ujumbe wake, Moses Kuria amemwambia Gachagua:

“Ni zamu yako sasa, ndugu yangu. Ninasubiri.”

Changamoto hiyo imekuja wakati ambapo mjadala kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa Gachagua na uwezekano wa ushirikiano au makubaliano ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka 2027 ukiendelea kuvuta hisia nchini humo.

Magazeti leo Agosti 8, 2026
08/08/2026

Magazeti leo Agosti 8, 2026

07/08/2026

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewahakikishia ulinzi wa kutosha wasanii, mashabiki na wapenzi wote wa muziki wa Bongofleva kuelekea tamasha la kihistoria la kuadhimisha miaka 30 ya sanaa hiyo.

​Hayo yanajiri ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika katika eneo la The Climax, Wilaya ya Ilemela, tarehe 8 Agosti 2026.

​Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wasanii nje ya viunga vya ofisi yake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, ameeleza kuwa mifumo yote ya kiusalama imeimarishwa.

​“Hali ya usalama mkoani hapa ni shwari na imewekewa ulinzi imara kuelekea tamasha hilo kubwa litakalokusanya maelfu ya wakazi na wageni ndani ya Jiji la Mwanza,” amesema Kamanda Mutafungwa.

​Kamanda Mutafungwa amesisitiza kuwa mikakati thabiti imeshawekwa ili kuhakikisha kuwa tamasha hilo linaanza na kumalizika kwa amani, utulivu na salama.

​Kamanda Mutafungwa, ambaye pia alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wasanii wa Bongofleva waliomtembelea ofisini kwake, alibainisha kuwa ulinzi umeimarishwa maeneo ya ndani na nje ya eneo la tukio, maeneo ya maegesho ya magari, pamoja na barabara zote kuu zinazoingia na kutoka eneo hilo.

​Hatua hizo zote zinalenga kulinda usalama wa wananchi na mali zao, ili kutoa fursa kwa kila mwananchi kufurahia burudani hiyo bila hofu yoyote.

​Hata hivyo, Kamanda Mutafungwa ametoa onyo kwa baadhi ya watu wanaoshiriki katika shughuli za ulinzi, wakiwemo mabaunsa, kutotumia nguvu kubwa dhidi ya watu watakaotuhumiwa kutenda uhalifu, badala yake wawasilishe au kutoa taarifa kwa askari wa Jeshi la Polisi watakaokuwa wanaimarisha ulinzi eneo hilo.

​Pia, Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi na mashabiki wote kutoa ushirikiano kwa askari watakaokuwa kazini, kufuata sheria za usalama barabarani, na kutoa taarifa za haraka kuhusu viashiria vyovyote vya uhalifu kupitia namba za dharura au kwa askari aliye karibu.

07/08/2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema Serikali imetoa Shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kisasa la chuma katika Mto Nyameni, uliopo Kata ya Ulaya, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Prof. Shemdoe ametoa taarifa hiyo Agosti 6, 2026, alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA). Amesema ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 30, 2026.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 30 linatarajiwa kuboresha usafiri na usafirishaji kati ya Kata za Zombo, Nyameni na Ulaya. Pia litawawezesha wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi kwenda sokoni pamoja na kupata huduma muhimu za kijamii k**a afya na elimu.

Serikali imeeleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa maeneo hayo kwa kuboresha miundombinu na kurahisisha mawasiliano.

07/08/2026

Mahak**a ya New Mexico nchini Marekani imeiamuru kampuni ya Meta kulipa dola milioni 567 (takriban Shilingi trilioni 2.5 za Tanzania), baada ya kubaini kuwa kampuni hiyo haikutoa onyo la kutosha kuhusu hatari zinazoweza kuwakumba watoto wanaotumia majukwaa yake.

Jaji Bryan Biedscheid alisema Meta ni "kero kwa umma" na akaagiza fedha hizo zielekezwe katika mfuko maalum wa kusaidia kupunguza madhara yanayohusiana na usalama wa watoto. Uamuzi huo ni miongoni mwa hatua kubwa zaidi za kisheria zilizowahi kuchukuliwa dhidi ya kampuni hiyo katika suala la ulinzi wa watoto mtandaoni.

Malipo hayo yanaongezeka juu ya dola milioni 375 ambazo Meta ilikuwa tayari imeamriwa kulipa katika kesi hiyo, na kufanya jumla ya fidia kufikia dola milioni 942. Mahak**a pia ilisisitiza umuhimu wa kudhibiti madhara ya kisaikolojia na unyonyaji wa watoto yanayoweza kuchochewa kupitia mitandao ya kijamii.

Meta, inayomiliki Facebook, Instagram, WhatsApp na Threads, imepinga uamuzi huo na kutangaza kuwa itakata rufaa. Kampuni hiyo imeeleza kuwa inaendelea kuimarisha mifumo ya usalama kwa watoto na kupambana na watu wenye nia mbaya pamoja na maudhui hatari kwenye majukwaa yake.

Kesi hii ni sehemu ya maelfu ya mashauri yanayoikabili Meta nchini Marekani yanayohusu usalama wa watoto, huku mjadala kuhusu wajibu wa kampuni za mitandao ya kijamii katika kulinda watumiaji ukiendelea kushika kasi.

Magazeti ya leo Agosti 7, 2026.   komenti kusoma yote.
07/08/2026

Magazeti ya leo Agosti 7, 2026. komenti kusoma yote.

06/08/2026

Mfanyabiashara na Mkazi wa Butimba jijini Mwanza, Elizabeth Chacha Mugusuhi (30), amepandishwa kizimbani katika Mahak**a ya Mwanzo Mkuyuni, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, leo Agosti 6, 2026 na kuhukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili katika Kesi ya Jinai Namba 1012/2026.

​Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa alitenda makosa hayo Julai 25, 2026 katika eneo la Kituo cha Polisi Nyegezi, ambapo kosa la kwanza ni kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma kinyume na kifungu cha 122(a) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 Marejeo ya mwaka 2023. Kosa la pili ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 cha sheria hiyo hiyo.

​Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahak**a ya Mwanzo Mkuyuni, Mhe. John Mgonya, Mwendesha Mashtaka Sajenti Doroth Mauma amesema mshtakiwa alitenda makosa hayo akijua wazi kuwa ni kinyume na sheria.

​"Wewe Elizabeth Chacha Mugusuhi, mnamo Julai 25, 2026 majira ya saa 8:00 usiku katika maeneo ya Kituo cha Polisi Nyegezi, ulitoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi kuwa umetekwa na watu wasiojulikana huku ukijua kuwa ni kosa kisheria. Pia, siku hiyo hiyo majira ya saa 8:00 usiku, ulijipatia kiasi cha Sh 800,000/= kwa njia ya udanganyifu ulizoomba utumiwe kwa madai kuwa umetekwa," alisema Sajenti Doroth.

​Hata hivyo, mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka mawili yanayomkabili, amekiri kutenda makosa hayo na kuiomba mahak**a impunguzie adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na ana watoto wadogo wanaomtegemea.

​Akitoa hukumu katika kesi hiyo, Mhe. Mgonya amesema kwa kuwa ni makosa yake ya kwanza na hakuisumbua mahak**a kwa kukiri kosa, mahak**a imeona impatie adhabu itakayokuwa fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia k**a hiyo.

​"Mahak**a inatoa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi sita kwa mshtakiwa chini ya Kifungu cha 2(1)(a) cha Sheria ya Mahak**a za Mahakimu, Sura ya 11 Nyongeza ya III Marejeo ya mwaka 2023, pamoja na kufanya kazi za jamii.

06/08/2026

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, ameomba radhi kufuatia dosari zilizojitokeza katika mpango uliolenga kuuza sehemu ya hisa za haki za kibiashara za mashindano ya FIFA kwa wawekezaji binafsi kupitia kampuni tanzu ya FIFA Forward Enterprise (FFE). Licha ya kukosolewa vikali, viongozi wakuu wa FIFA wameendelea kumuunga mkono na kuthibitisha kuwa ataendelea kuiongoza taasisi hiyo.

Infantino, aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa FIFA mwaka 2016 baada ya kuondoka kwa mtangulizi wake Sepp Blatter kufuatia kashfa za ufisadi, ameiongoza FIFA kwa takriban muongo mmoja. Kwa sasa anajiandaa kuwania muhula wa nne katika uchaguzi wa urais wa FIFA unaotarajiwa kufanyika Machi 2027.

Mzozo huo ulianza baada ya kubainika kuwa Infantino alipendekeza kuanzishwa kwa kampuni ya FFE, ambayo ingeruhusu wawekezaji binafsi kununua hisa katika haki za kibiashara na tiketi za mashindano makubwa ya FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia la Wanaume na la Wanawake.

Mpango huo ulipingwa vikali na UEFA pamoja na baadhi ya viongozi wa ndani ya FIFA kwa madai kuwa uliandaliwa kwa siri, haukuwa na uwazi wa kutosha na ungeweza kuhatarisha uhuru wa usimamizi wa mashindano hayo.

Katika kikao cha dharura kilichofanyika jijini Rabat, Morocco, Infantino na Katibu Mkuu wa FIFA, Mattias Grafstrom, walikiri kuwepo kwa mapungufu katika namna mpango huo ulivyoandaliwa na kuwasilishwa bila ushirikishwaji wa kutosha wa wadau.

Viongozi hao pia walituma barua ya kuomba radhi kwa vyama wanachama wa FIFA, wakiahidi kuwa makosa k**a hayo hayatajirudia. Aidha, FIFA ilisisitiza kuwa, licha ya dosari hizo, taratibu zake za utawala hazikukiukwa.

Hata hivyo, shinikizo dhidi ya Infantino linaendelea kuongezeka, huku UEFA ikitangaza kupoteza imani na uongozi wake na baadhi ya vyama vya soka barani Ulaya vikiondoa uungwaji mkono kwa azma yake ya kuwania muhula wa nne mwaka 2027.

Pamoja na changamoto hizo, Infantino bado anaungwa mkono na mataifa kadhaa, hususan kutoka Afrika na Asia.

Address

Nyamagana
Mwanza
994

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Famara Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Famara Media:

Shortcuts

Share