Kijana NA Maisha

Kijana NA Maisha KIJANA AKIJITAMBUA BASI KIZAZI CHOTE HAKITAJUTA UWEPO WAKE HAPA DUNIANI. THE YOUTH'S SELF-DETERMINATION WILL MAKE THE WHOLE GENERATION BE PROUD OF HIM/HER.

05/03/2022
USIJIRINGANISHE MAISHA YAKO KWA WENGINE. HAKUNA ULINGANIFU KATI YA JUA NA MWEZI MAANA KILA KIMOJA HUNG'AA KWA WAKATI WAK...
06/12/2019

USIJIRINGANISHE MAISHA YAKO KWA WENGINE. HAKUNA ULINGANIFU KATI YA JUA NA MWEZI MAANA KILA KIMOJA HUNG'AA KWA WAKATI WAKE.
"Tuishi maisha yetu HALISI tukisimamia malengo yetu pasi kuwa na mtazamo HASI."

_*NDOTO ZA MABINTI WENGI NI HARUSI.*__*Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la N...
12/10/2018

_*NDOTO ZA MABINTI WENGI NI HARUSI.*_

_*Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi.*_

_*Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku.*_

_*Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele.*_

_*Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon.*_

_*Ndio maana wengi wanakazana kuchangia harusi za wenzao na kushiriki hata kushona sare ili na yeye kwenye harusi yake wamchangie.*_

_*Inasikitisha sana kwamba wengi hawafikirii maisha ya Ndoa.*_

*Hawajiulizi maswali ya msingi k**a;*

*JE NIKO TAYARI KUWA MKE WA MTU?*

*NIKO TAYARI KUJIDHABIHU KWAAJILI YA FURAHA YA MTU MWINGINE?*

*JE' NIKO TAYARI KUSALIMISHA MATAKWA YANGU KUFANYA MATAKWA YA MTU MWINGINE?*

*JE' NIKO TAYARI KUWA MAMA NA KULEA FAMILIA?*

*JE' NIKO TAYARI KUPIGANIA NDOTO ZA MTU MWINGINE?*

*JE' NIKO TAYARI KUAMBATANA IKIBIDI KUHAMA MJI NINAOPENDA NA KWENDA KUISHI NISIKOPENDA ILI KUTIMIZA NDOTO YA MUME WANGU?*

_*Niko tayari kuingia ukoo mwingine na kuufanya kuwa ukoo wangu, watu wake wawe watu wangu na Mungu wao awe Mungu wangu?*_

_*Ikitokea umeolewa na Mume wako akapata shida ghafla mfano Ugonjwa na akashindwa kutunza familia, una mbinu gani mbadala ya kuendesha maisha yenu mpaka atakapopona na kusimama tena?*_

_*Una uwezo wa kubeba majukumu k**a Mama maana kuzaa ni jukumu lingine kabisa?*_

_*Tabia yako vipi? Inafaa kuwa mke wa mtu? Au unahitaji muda kwanza na uhuru ujirushe ukichoka ndio utulie uolewe?*_

_*Kuna msemo "Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke" ukijiangalia wewe una uwezo wa kumshauri mtu akafanikiwa?*_

_*Na hilo tunalipima kwa kuangalia ni nini ambacho binafsi umefanikisha katika maisha yako.*_

_*Moja jumlisha moja huzaa mbili, wewe una moja gani ya kuchanganya na moja aliyonayo mume wako mkazalisha mafanukio? Au unaenda kuwa Mama wa Nyumbani na mzigo.*_

_*Ulishwe, uvishwe, upewe kila kitu wakati hakuna unachozalisha?Nadhani kuna mambo ya maana ya kufanya, kupanga na kujiandaa kabla hujawaza rangi ya harusi (Wedding colour), keki ya ngazi saba na hotel ya kwenda Honeymoon.*_

*Me nimemaliza.*

_*Usije ukaishia kufurahia harusi na baada ya mwaka ukaanza kutafuta Washauri wa Ndoa.*_

*Think before U take Decision*

PAMOJA NA SIMBA WAKALI KUWEPO MWITUNI swala au twiga hajawahi fikilia kuhama pori na kuingia kwenye makazi ya watu. Wewe...
15/09/2018

PAMOJA NA SIMBA WAKALI KUWEPO MWITUNI swala au twiga hajawahi fikilia kuhama pori na kuingia kwenye makazi ya watu. Wewe kijana mwenye kukata tamaa sababu ya changamoto zinazokuzunguka usithubutu kujuta kuwepo katika ulimwengu huu. Kupitia changamoto mafanikio hupatikana. Kumbuka mafanikio ya haraka ni rahisi kwenda mrama sababu yamekosa msingi thabiti. Tumia URENGE au FIKRA YAKINIFU pale unapoamua kufanya jambo fulani. Kuwa na mipango yenye uwezo wa kusitawisha mti wa mafanikio uzaao matunda kwa muda mrefu. Tazama uwezo wako ukimshirikisha Mungu na si wanadamu hasa wale wenye shauku ya kuona ukihaha kwa kufeli. Jitambue UWEZO WAKO na tambua kuwa hakuna lisilowezekana chini ya jua. Mwenyezi Mungu akubariki wewe kijana uaminiye KUFANIKIWA na SI KUSHINDWA.

UNAWEZA KUSHINDWA KUDHIBITI KILA HALI INAYOJITOKEZA NA MATOKEO YAKE, ILA UNAWEZA KUDHIBITI MTAZAMO WAKO na NAMNA UNAVYOP...
10/08/2018

UNAWEZA KUSHINDWA KUDHIBITI KILA HALI INAYOJITOKEZA NA MATOKEO YAKE, ILA UNAWEZA KUDHIBITI MTAZAMO WAKO na NAMNA UNAVYOPAMBANA NAO DHINA YA MIPANGO ULIYOPANGA KUFANIKISHA

NAWAPENDA SANA DADA ZANGU ila kero yangu ni moja tu. Mnakubali kirahisi pesa itoe UTU wenu na kujitia UTUMWA. Hebu pata ...
29/11/2017

NAWAPENDA SANA DADA ZANGU ila kero yangu ni moja tu. Mnakubali kirahisi pesa itoe UTU wenu na kujitia UTUMWA. Hebu pata wazo la kuwa mwanaume hakuumbwa na damu ambayo akisogea ATM pesa zinatoka. Fahamu kitu kimoja, yeyote aliyetafuta pesa kwa uchungu lazima nae atakuwa na uchungu nayo. Sasa wewe ukileta masihala pasipo jali jasho la huyo mwanaume alitaabika kuzisaka hakika utaishia kuwalaani wanaume wote. Jali utu wako, na heshimu jasho la mtu. Tukijikita kufikilia ni namna gani familia itasonga mbele, UMATEMATE utapungua. Nasema haya nikiumizwa na vitendo wanavyofanyiwa wanawake eti kisa PESA. MUNGU AWABARIKI MBADILIKE MITAZAMO AMBAYO SI RAFIKI KWA UTU WA MWANAMKE.
HESHIMA KWA WANAWAKE WOTE WANAOHESHIMU UTU WAO!

"VUNJA VITU VYOTE ILA USIUVUNJE MOYO WA KUPIGANIA MAFANIKIO" UKITAMBUA kusudi la Mwenyezi Mungu kukuleta hapa duniani ba...
07/11/2017

"VUNJA VITU VYOTE ILA USIUVUNJE MOYO WA KUPIGANIA MAFANIKIO"
UKITAMBUA kusudi la Mwenyezi Mungu kukuleta hapa duniani basi hakuna haja kuumiza kichwa hasa baada ya kushindwa kwa mambo fulani ambayo ulidhani utayapata. Ni kheri kuwa na tumaini maana hatujui thawabu ya kesho ambayo ni fumbo na mfumbuzi ni Mungu pekee. Mioyo ya wanadamu daima hukatisha tamaa. Baki kuwa IMARA kifikra, kimtazamo ili hali ukimtumainie yeye aliyeleta ULIMWENGU HUU ....!

KIJANA KATIKA KUTAFUTA MAFANIKIO
26/08/2017

KIJANA KATIKA KUTAFUTA MAFANIKIO

KUJIAMINI NA IMANI NI NGUZO MUHIMU KATIKA MAFANIKIO ENDELEVU
Katika maisha yetu hasa kwetu vijana, binafsi huwa najiuliza; ni aina gani ya mafanikio ambayo ni vema niyafikie? Je, mafanikio hayo yatadumu kwa muda gani? Ni vitu gani vyaweza kuwa msingi wa kufikia malengo hasa yale ambayo ni HALALI/STAHIKI, ENDELEVU na YENYE MANUFAA KWANGU NA KWA JAMII NZIMA. La hasha, kuna vitu ambavyo YATUPASA tuvitazame kwa umakini na tuvipiganie.

¤ MAFANIMIO HALALI: hapa namaanisha kufanikiwa kitu kile bacho ni stahiki kwako na hakina jicho baya kwa wale ambao wanamuamini mwenyezi Mungu.
Maana tukisema tuthaminishe uhalali kwa kutumia jicho la mwanadamu; tutapoteza mwelekeo.
Hapa ndipo tunakuta mafanikio ambayo yana manufaa kwa mtu binafsi na kwa jamii kwa ujumla. Haya ndiyo mafanikio halali.
Mfano, mwingine atajiuliza kwani ukimpata mke au mume halali/mwema jamii inanufaika vipi? Ni hivi, kupitia mke au mume mwema hakuta kuwa na mtoto kibaka. Jamii itakuwa na usalama.

¤ MAENDELEO ENDELEVU (sastainable development); hapa namaanisha maendeleo ambayo kizazi cha kesho kitanufaika kwa mafanikio husika. Swali la msingi ni Je, mafanikio yako yata/yanadumu kwa muda gani?

¤ KUJIAMINI na IMANI: Chachu ya kufikia malengo ambayo ni Halali na Endelevu ni kujiamini na imani. Ukiwa unajiamini na una imani mambo mengi yatafanikiwa. Kujiamini hakuendani na uwoga wa kufanya jambo ambalo unaona lina manufaa lakini wasita kisa watu watakucheka au watakudharau. Amini njia ya mafanikio kwa asilimia kubwa haiwapendezi macho ya wanadamu. Kuwa na ujasili wa kupita njia hiyo kwani ni k**a DAWA ambayo huwa chungu ila HUPONYA.
Ni mawazo yangu,
(Meckson Kaboga)
KARIBU KWA MAWAZO YAKO!

Address

Plot No. 186, Block "F" Nyegezi - Mwanza
Nyegezi
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kijana NA Maisha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share