Lazaro Samwel

Lazaro Samwel Nawasaidia Wafanyabiashara Kupata Wateja Na Kuongeza Mauzo x10 Kwenye Biashara Zao Hii ni ukiweka pembeni MAKAMPUNI niliyofanya nayo kazi.

Mtatuzi wa tatizo la kukosa wateja na kushindwa kuongeza mauzo ya kuridhisha kwenye biashara yako. Toka mwaka 2019 nilipoanza madarasa BINAFSI ya wafanyabiashara nimeshafanya kazi na zaidi ya wafanyabiashara 300 na kuwasaidia kupata wateja na kuongeza mauzo ya biashara zao ndani na nje ya mitandao yao ya kijamii. Hata wewe naweza kukusaidia kwa hili ndani ya siku 7-30 na ukaanza kuona mabadiliko m

azuri kwenye biashara yako. Unaruhusiwa kabisa kuomba kurudishiwa hela yako endapo hutaona mabadiliko yoyote kwenye biashara yako kwa mafunzo utakayopatiwa

Ungependa kuwa miongoni mwao?

20/02/2026

SHARE na SAVE

Follow ili usipitwe na masomo k**a haya.

19/02/2026

Saikolojia ya Sekunde 7 za Kwanza, Jinsi ya Kuanza na Mteja

Je, unajua kuwa mteja anapoingia kwenye ofisi yako au anapopokea simu yako, anachukua sekunde 7 TU kukuweka kwenye kundi la "Wataalamu" au "Tapeli"? 😱

Hizi sekunde 7 zinaweza kukupa dili au kukufanya upoteze mteja tajiri bila wewe kujua!

Sasa ndani ya sekunde 7 tuu hakikisha unatumia sehemu hizi 4 za mwili wako vizuri kuonekana Mtaalamu...

1. Macho na Tabasamu (The Visual Hook)

Kabla hujasema neno, macho yako na tabasamu lako vishazungumza.

Mteja anahitaji kuona unampokea kwa furaha, siyo k**a mtu unayemsumbua.

Tabasamu ni lugha ya kimataifa inayosema: "Uko mahali salama."

2. Salamu yenye Nishati (The Greeting Energy )

Epuka salamu zilizochoka k**a "Habari yako?".

Badala yake, tumia salamu yenye nguvu na uchangamfu.

Sema: "Karibu sana [Jina la Kampuni], naitwa [Jina Lako], nimefurahi kukuona leo!"

Salama hii ni k**a mteja unamjua na sio mgeni hata k**a ni mara ya kwanza kuja ofisini kwenu.

3. Focus iwe kwake, siyo kwenye simu yako

Sekunde 7 za kwanza, mteja anapaswa kuwa ndiye "Mfalme".

Ukiacha kumsikiliza ili uandike meseji au uongee na mfanyakazi mwenzako, umeshabomoa daraja la uaminifu.

4. "Body Language" (Lugha ya Mwili)

Simama wima, elekeza kifua chako kwa mteja.

Hii inaonyesha kuwa upo tayari kumhudumia na unajiamini na unachokifanya.

KOSA KUBWA..:

Wafanyakazi wengi wanamsubiri mteja aanze kuongea.

Hapana! Wewe ndiye mwenyeji.

Wewe ndiye unayeongoza mchezo.

Mteja hachezi na bidhaa yako kwanza, anacheza na "Vibe" lako.

Ukishindwa sekunde 7 za kwanza, utatumia saa nzima kujitetea ili akuamini.

JE, TIMU YAKO INAJUA HILI?

K**a biashara au taasisi yako inapoteza wateja wakati mna bidhaa nzuri, tatizo linaweza kuwa ni hizi sekunde 7.

Nitumie ujumbe hapa k**a unahitaji niwafundishe vijana wako sanaa ya kumpokea mteja na kuifanya ofisi yako iwe sumaku ya wateja!

19/02/2026

LIKE na SHARE

Follow ili usipitwe na masomo k**a haya.

Address

Nyegezi
0753616584

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lazaro Samwel posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Lazaro Samwel:

Share