SAUTI MEDIA

SAUTI MEDIA For any thing about business advertising you're welcome contacts me via #0764313742 Mr shomy

"Katika fitina kiingilio ni husda yako, katika umbeya kiingilio ni maskio yako. Penye busara kiingilio ni akili yako. Pe...
16/05/2022

"Katika fitina kiingilio ni husda yako, katika umbeya kiingilio ni maskio yako. Penye busara kiingilio ni akili yako. Penye ibada kiingilio ni imani yako. Msibani kiingilio ni huzuni yako na harusini kiingilio ni mchango wako. Utaingia kule ambako kiingilio chako kinatosha."

 # kitaa knowledge kwa kawaida inachukua siku 21 kwa my kujenga Tabia mpya na kuiacha ya zamani, lakini cha kusikitisha ...
14/01/2021

# kitaa knowledge

kwa kawaida inachukua siku 21 kwa my kujenga Tabia mpya na kuiacha ya zamani, lakini cha kusikitisha watu hukata tamaa siku Za mwanzoni tu.
Kuacha Tabia ulioizoea na kujenga Tabia mpya sio kitu rahisi lakini Ni Jambo linalowezekana.
# mfano, mtu akinunua viatu vipya , siku za mwanzoni vitambana lakini baada ya muda kam wiki moja ua mbili vitamkaa vizuri na atasahau K**a vilikuwa vinambana.
Na ndo hivyo ilivyo katika kujenga Tabia mpya , mwanzo huwa ngumu lakini baadae huwa kawaida , na utasahau K**a ulikuwa unapiga nyeto, mvivu kuamka, mwizi, mchoyo, mzembe n.k

# mawazo chanya huwa na matokeo chanya, badilisha wazo hasi kwa wazo chanya

NGUVU YA UTHUBUTU:Uthubutu ni nini?∆ Uthubutu ni hali ya kuchukua hatua za makusudi kufanya jambo furani, na kupata mato...
11/01/2021

NGUVU YA UTHUBUTU:

Uthubutu ni nini?

∆ Uthubutu ni hali ya kuchukua hatua za makusudi kufanya jambo furani, na kupata matokeo ya hatua hizo.

∆ kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kumjengea mtu uwezo wa kuthubutu nayo ni k**a ifuatavyo.

1. Ujasiri - katika matokeo ya uthubutu mtu unaweza kupata matokeo chanya ama matokeo hasi kwa mfano mtu anaweza kuthubutu kuingia kwenye biashara ama akapata faida ama hasara, sasa ili mtu uweze kufanya jambo furani inakulazimu uwe na ujasiri wa kufanya jambo lenyewe na kuwa na mtazamo chanya kwenye jambo hilo..

2. Kutafuta taarifa sahihi juu ya jambo unalotaka kufanya(research)
-kwenye kuamua kufanya jambo furani taarifa za awali juu ya jambo hilo ni muhimu sana kwa mfano unataka kuthubutu kuingia kwenye kilimo inakubidi utafute taarifa za muhimu kwenye kilimo ili ujue zao unalotaka kulima linakubali kwenye hali ipi ya hewa, pembejeo gani zinatumika, soko lake lipo wapi n.k kufanya hvo kutakuongezea uwezo wa kuamini unaweza kufanya na kufanikiwa kwa sababu utaweza kupima gharama za uzalishaji na faida utayo pata(total cost vs total product)..

3. Kufanyia kazi ndoto zako.
-jambo kubwa ambalo linafanya watu washindwe kuthubutu nikuwa na ndoto za mafanikio na kuziona k**a ni ndoto kwa hivi kufikiri labda kunamuujiza utatokea kutimiza ndoto hizo. Kiualisia ndoto ya mafanikio ni fursa ambayo mtu anaiona kutokana na sehemu anayotoka mfano sehemu unayotoka kunashida ya maji basi ukawa na ndoto ya kununua matanki makubwa ya kuifadhi maji kipindi cha masika na uyauze kiangazi. Ndoto k**a hyo unatakiwa uone inawezekana kwahvi kinacho hitajika ni uthubutu wa kufanya ndoto iwe fursa..n.k

∆ Kiukweli kuthubutu kwenyewe kunahitaji uthubutu ko ili uweze kuwa na mafanikio THUBUTU KUTHUBUTU kwa faida zifuatazo:-

∆ Jambo kubwa ambalo tunatakiwa kujua ni kwamba mungu aliumba dunia na fahali zake kwahivi kila tunacho kihitaji tayari kipo duniani. Ukitaka kujua ukweli huo fatiria kizazi cha zamani ambacho wenyewe fursa ya kuishi walikuwa wakitegemea mimea na wanyama lakini badae vile vitu ambavyo walikuwa wanachezea k**a dhahabu vikajakuwa ni vitu vya thamani na tunavitumia kuboresha maisha kwahiyo ubunifu binafsi unatakiwa kwenye uthubutu wako juu ya jambo furani ambapo utapata kitu kipya na kukufanya uwe wa kipekee kwenye bidhaa yako na utajizidishia wahitaji(demands) na kupata faida zaidi(super normal profit)..

∆ Nguvu ya uthubutu pia inakupa uwezo wa kujiamini kwenye kutoa maamzi juu ya jambo furani, unaweza kuwa kijana na umekuwa umekuta kwenye familia yenu kuna mila au tabia furani mfano ubaguzi wa kijinsia kwenye shughuli za kiuchumi ambayo umeona inakwamisha maendeleo kwenye familia ko k**a unanguvu ya uthubutu unaweza kuwa na ujasiri wa kutoa ushauri maamzi na kufanya wazazi waelewe na kufanya mabadiliko kwenye familia na kufanya maendekeo kwenye familia na hata jamii kiujumla..

∆ Kuthubutu kunaweza kukupatia jina la kipekee(brand), ni ukweli usiopingika kwamba kutafuta umaarufu ni huruka ya kibinadamu na wala siyo dhambi, na nikweli kwamba mtu mwenye umaarufu anafuatwa na fursa nyingi hata k**a hajasoma lakini utaona kunamakampuni makubwa yanafanya mkataba naye ie. Plutnum diamond. Ko tunatakiwa kujua umaarufu hauji pasipo kuthubutu kufanya jambo furani k**a unahisi unakipaji chochote inakulazimu uthubutu kuwaonesha watu kipaji chako, k**a wewe ni msomi akikisha jamii inatambua taaruma yako kwa sababu jamii ndio mwajili wako wa kwanza ndipo nafasi zingine zinafuata..

∆ Kuthubutu pia ni mlango wa baraka zako, kunamtu anaweza kuwa amekaa anatazama mtu furani alivyo fanikiwa na kusema furani kabarikiwa na Mimi sijabarikiwa kiukweli huwezi kuziona baraka pasipo kuthubutu kufanyajambo ukishalima utaona mazao yanavyositawi ndipo utasema hakika naziona baraka za mungu. Na kwenye biashara kaa jua hakuna ufanyabiashara aliye zaliwa mfanyabiashara mkubwa Bali wote wameanza wadogo , wakawa wakati hatimae leo wafanyabiashara wakubwa nao wanafurahia baraka za mungu ambazo wasinge thubutu kuanza na ule mtaji mdogo wasinge ziona

Sauti inatosha au niongeze
23/12/2020

Sauti inatosha au niongeze

31/05/2020
Sauti media tunapenda kuwatakia wa Tanzania wote siku kuu njeEMA ya idd El fitri
24/05/2020

Sauti media tunapenda kuwatakia wa Tanzania wote siku kuu njeEMA ya idd El fitri

Nlipokua mdogo nilikua namuona Mama akichambua maharage,alkua anaweka mazima kwenye sufuria kwa ajili ya kuyapika na mab...
13/05/2020

Nlipokua mdogo nilikua namuona Mama akichambua maharage,alkua anaweka mazima kwenye sufuria kwa ajili ya kuyapika na mabovu anayatoa Kisha anayatupa jalalani..
💦Cha kushangaz mvua ikinyesha maharage yaleyale mabovu ndio yakua ya kwanz kuota na kuchipua.,.,yanatupwa yakiwa mabovu yasiyofaa lakin yanaota Kisha yanatoa maharage mengine mazur na Bora zaidi kuliko yalvotupwa mwanzo yakiwa mabovu...
💦 hii nmejifunza kwamba watu wanavokuona Ni tofaut kabisa na MUNGU anavyokuona inawezkana ukajiona maharage mabovu Leo lakn hakika mvua ya Bwana ikikunyeshea utaota na kustaw utakua na thaman zaidi ya vle unavyofikilia..
💦 Unahtaj uvumilivu na kujua kusudi la MUNGU na mawazo ya MUNGU tofaut na ya mwanadam.....Amen.🙏 mbarikiwe watu wa MUNGU..mch Humphrey mtendah DSM

Huwezi kuwa na mtazamo CHANYA kwenye maisha k**a wewe kila siku una jicho la kuona MABAYA tu.Umeshawahi kuwa na mtu kwen...
05/05/2020

Huwezi kuwa na mtazamo CHANYA kwenye maisha k**a wewe kila siku una jicho la kuona MABAYA tu.

Umeshawahi kuwa na mtu kwenye mahusiano halafu kila siku anakukosoa kwa mabaya lakini hata hukumbuki mara ya mwisho akisifia ZURI ulilolifanya?
Au kuna mtu uko naye ofisini kila siku ni kusema kwa sauti mambo yanapoenda mrama ila hajawahi hata “kuapreciate” kitu kizuri?
Njia mojawapo ya kujenga mtazamo chanya (Positive Attitude) kwenye maisha yako ni kujilazimisha kutafuta vitu vya KUSIFIA na KUSHUKURU.

Hata katikati ya MAGUMU unatakiwa kutafuta jambo ambalo linaweza kukusababisha kushukuru na kusifia.

Ukweli ni kuwa kila siku kuna kitu ambacho unaweza kukipata na ukashukuru au ukasifia.

Ila UTAKIONA tu k**a UTAKITAFUTA.

Leo anza kutafuta kitu cha kushukuru kwanza.

Kisha tafuta angalau watu WATATU ambao utawaambia maneno mazuri ya KUWASIFIA na KUWATIA MOYO.

Mara nyingi tunadhani tukifanya hivyo TUNAWASAIDIA wao ila ukweli ni kuwa TUNAJIJENGA wenyewe MTAZAMO CHANYA.

Watu wengi sana wanapoanza kufanya kitu kwa mara ya kwanza wanakutana na “kuzodolewa” . Kuna watu ni k**a wanasubiri ufa...
26/04/2020

Watu wengi sana wanapoanza kufanya kitu kwa mara ya kwanza wanakutana na “kuzodolewa” . Kuna watu ni k**a wanasubiri ufanye kitu ili “wakuzodoe” na ukate tamaa. Kitu cha ajabu ni kuwa wao wenyewe huwa hakuna wanachofanya.
Kwa sababu ya hii HOFU ambayo wengine wamekutana nayo na wengine wameona baadhi ya watu wakiipitia,kuna watu wengi sana ambao wanaogopa kabisa KUFANYA KITU.
Kuna mtu unasoma hapa leo na kuna BIDHAA,BIASHARA au WAZO umekuwa unaghairisha kila siku kulifanyia kazi kwa sababu unaogopa “Utazodolewa”.Matokeo yake,kila siku unataka kitu chako kikamilike 100% kabla HAUJAANZA.
Moja ya somo bora nililowahi kufundishwa ni kwamba “IMPERFECT DONE is better than the PERFECT NOT DONE” (Ni bora kufanya kitu chenye mapungufu kuliko kusubiri kikamilike na ukaishia kutokufanya). Kumbuka njia nzuri ya kujifunza, ni kufanya na kugundua wapi unatakiwa kuboresha. Usipofanya HAUTAJUA namna bora ya kuboresha.
Baada ya somo hili nilifundishwa lingine kuwa “NOTHING WORKS BEST AT THE THE FIRST TIME”(Hakuna kinachofanikiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa mara ya kwanza). Ukianza ni k**a mtoto kutembea,utakosea kwenye mambo mengi ila hiyo haimaanishi kuwa HAUTAFANIKIWA. Mtoto angeacha kujaribu kutembea kwa sababu ya kuogopa KUZODOLEWA angejikuta HAWEZI TENA KUTEMBEA.
Kumbuka WAZODOAJI HAWAISHI na WANAZALIWA UPYA kila siku.Anza KUFANYA na USIOGOPE KUZODOLEWA.Kumbuka WAZODOAJI wengi huwa HAWAFANYI kitu na wanataka MFANANE.Umeshawahi kukutana na WAZODOAJI?

Chukua japo dakika moja kumshukuru mwalimu wako
25/04/2020

Chukua japo dakika moja kumshukuru mwalimu wako

Have a nice day
11/09/2018

Have a nice day

Address

Tabora

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SAUTI MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share