28/11/2023
*πSOMA SALA HII π*
π Bwana Yesu , ninakuja mbele zako .
Ninakuomba unisamehe maana nimejitamkia maneno mabaya ya kushindwa.
πNirehemu ee BWANA , maana sikukujua lakini sasa nimejua makosa yangu juu ya maneno mabaya niliyojitamkia.
π Nakuomba uyafute maneno mabaya niliyojitamkia katika maisha yangu , katika jina la Yesu .
πNinaomba uwasamehe hata wale walionitamkia maneno mabaya juu ya familia yangu , biashara zangu, ndoa yangu , elimu yangu n.k
Ee Mungu uyafute maneno yao mabaya , waliyonitamkia kwa kujua na kwa kutokujua. Kwa damu ya Yesu futa maneno yao kuanzia sasa , maana imeandikwa:
π¨π»βπ»π 10 Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.
Zaburi 33 :10
11 Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
Zaburi 33 :11
Nami nakuomba maneno niliyotamkiwa uyafutilie mbali katika maisha yangu , familia yangu , ndoa yangu n.k bali neno lako likasimame daima maishani mwangu katika jina la Yesu .Amen
π₯Katika jina la Yesu , ninasema k**a ilivyoandikwa;
ππ¨π»βπ» 7 Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa.
Isaya 7 :7
Ninaamuru kila maneno mabaya kutokusimama katika maisha yangu na ndoa yangu , familia yangu , elimu yangu n.k
Maana imeandikwa:
ππ¨π»βπ» 10 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
Isaya 8 :10
πninayaamuru maneno yote mabaya niliyotamkiwa na niliyotamkiwa kuwa batili , katika jina la Yesu.
π₯Ninaamuru kila maneno mabaya na roho ya uharibifu kuachia maisha yangu , katika jina la Yesu nina yavua mavazi ya maneno mabaya kwa damu ya Yesu .
ππ¨π»βπ» 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Waebrania 9 :22
Asante Bwana Yesu kwa kuwa unasikia kuomba kwangu nami najikabidhi mikononi mwako sasa na hata milele .Amen
BIBILIA NI JIBU LAKO βοΈπππ